JK AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI - LEKULE

Breaking

21 Feb 2015

JK AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea. Pichani ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Nairobi Kenya ambapo alihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt.Shukuru Kawambwa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya  katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa  Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU


Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo  jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita

 "Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye.




Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.




Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo.
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia 6.

"Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri". 






No comments: