Mwigizaji nguli na muongozaji wa filamu za Kibongo, Jacob Steven
‘JB’, amesema kuwa pamoja na kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao,
anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema
kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashungulikia
wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.
JB alitoa ombi kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo
kwa wasambazaji lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale
wanapopeleka filamu zao sokoni.
“Rais wetu alitoa kauli kuwa atawashughulikia wale wote wanaohusika
na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini
hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie maana tunakufa masikini”
alisema JB.
No comments:
Post a Comment