I Coast yapanda katika orodha ya FIFA - LEKULE

Breaking

12 Feb 2015

I Coast yapanda katika orodha ya FIFA



Ivory Coast imepanda katika orodha ya shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kushinda kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu.

Equitorial Guinea waandalizi wa kombe hilo pia walipanda na kuorodheshwa miongoni mwa mataifa 50 bora duniani.

Kikosi hicho kilipanda nafasi 69 na sasa kiko sawa na Congo katika nafasi ya 49 baada ya kufika nusu fainali ya mchuano huo ijapokuwa kwa utata.

Kikosi cha timu ya Algeria bado kinaongoza barani afrika kulingana na orodha mpya ya FIFA 


Kikosi cha Ivory Coast kilipanda nafasi 8 juu hadi nafasi ya 20 ijapokuwa Algeria bado inasalia kuwa timu bora barani Afrika ikiwa katika nafasi ya 18..

Ndovu hao wameorodheshwa wa pili barani Afrika nyuma ya Desert Foxes,timu walioishinda katika robo fainali.

Timu ya Ghana ambayo ilicheza katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya walioibuka washindi Ivory Coast imepanda nafasi 12 hadi nambari 25.

Ujerumani yaendelea kuongoza katika orodha mpya ya fifa baada ya kushinda kombe la dunia 

Mataifa yalioshuka vibaya katika orodha hiyo barani Afrika ni Libya ilioshuka nafasi 35 hadi nambari 113 duniani.

Katika nafasi za kwanza ,Ujerumani bado inashikilia nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Argentina,Colombia,Belgium na Uholanzi katika nafasi ya 5.

Hakuna timu mpya zilizoingia katika orodha ya mataifa kumi 10 duniani.

Mataifa kumi bora barani Afrika: 1. Algeria 2. Ivory Coast 3. Ghana 4. Tunisia 5. Cape Verde 6. Senegal 7. Nigeria 8. Guinea 9. Cameroon 10. Congo DR

Mataifa kumi bora duniani 1. Germany 2. Argentina 3. Colombia 4. Belgium 5. Netherlands 6. Brazil 7. Portugal 8. France 9. Uruguay 10. Spain


No comments: