Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro
Meneja huyo ajulikanaye kwa jina la Bahati inaelezwa alienda kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo ndipo Bondia huyo alikataa kumlipa na kumshushia kipigo
No comments:
Post a Comment