Dr Magufuli amekagua njia ya kivuko cha MV Dar-es-Salaam kinachotarajiwa kufanya safari Dar es Salaam na Bagamoyo - LEKULE

Breaking

27 Feb 2015

Dr Magufuli amekagua njia ya kivuko cha MV Dar-es-Salaam kinachotarajiwa kufanya safari Dar es Salaam na Bagamoyo



Katika kukabiliana na adha ya foleni katika jiji la Dar es Salaam, waziri wa ujenzi Dr John Magufuli amekagua njia ya kivuko cha MV Dar-es-Salaam kinachotarajiwa kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani huku akiikaribisha sekta binafsi kushirikiana na serikali kuwekeza katika usafiri wa majini ili kupunguza adha ya foleni inayotajwa kusababisha hasara ya mamiliuoni ya shilingi katika uchumi wa nchi kwa siku.
Kutokana na hali hii, waziri wa ujenzi Dr Magfufuli akiongozana na viongozi wengine waandamizi wa wizara hiyo ameshiriki kikamilifu katika ukaguzi wa njia inayotarajiwa kutumiwa na kivuko hicho kwa kusafiri kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam kutoka magogono jijini Dar es Salaam hadi Mbegani Bagamoyo mkoani Pwani safari iliyotumia takriba saaa mbili na kuelezea namna kivuko hicho kitakavyokuwa cha manufaa kwa wananchi huku akiikaribisha sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji wa usafiri wa majini ili kupunguza msongamano jijini Dar es Salaam.

Aidha Mh Magufuli amesema kuwa mbali na kivuko hicho kutumika kwa ajili ya usafiri wa abiria pia kinaweza kutumika kama kivutio cha utalii.

Kwa upande wake meja jeneral Rogasian Laswai kutoka katika kikosi cha jeshi la wanamaji ambao wamepewa kandarasi ya kujenga vituo na maeneo ya kuegeshwa kwa kivuko hicho amesema kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ndani ya siku kumi zijazo ambapo rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wake.
Nao baadhi ya wananchi wameelezea namna kivuko hicho kinavyoweza kuwa faraja kwao kwa kuwaokolea muda huku wakitarajia bei ya nauli kuwa ya unafuu ambayo wananchi wote wanaweza kuimudu kwa ajili ya huduma kwa wananchi na si biashara.

Kivuko hicho cha kisasa kiliochotengenezwa nchini Denmark kina uwezo wa kubeba abiria 305 kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni nane fedha zilizotolewa na serikali ya Tanzania.

No comments: