Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa
habari zilizoenea mtaani kwamba kampuni hiyo imeuzwa ni za uzushi na
kuwataka Watanzania wazipuuze.
Kampuni
hiyo ambayo inamiliki Clouds FM, Clouds Tv na Choice FM ilidaiwa kuuzwa
kwa Rostam Aziz ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara maarufu na kada wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kusaga
(pichani) alisema habari hizo ambazo zilisambaa katika mitandao
mbalimbali ya kijamii zilisababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi na
viongozi wa Clouds pamoja na Watanzania kwa ujumla.
Alisema
habari hiyo imetengenezwa na watu walioamua kupoteza muda wao katika
mitandao ya kijamii, lakini wapo wanaovuna fedha nyingi kwa kupitia njia
hiyo ya mawasiliano.
Alisema
mara baada ya kuenea kwa habari hiyo, usumbufu mkubwa uliibuka kutokana
na watu wenye mapenzi mema na kampuni hiyo kuanza kuhoji juu ya taarifa
hizo kama zina ukweli.
“Clouds
Media Group ni kampuni iliyoanzia chini kwa ushirikiano wa watu wengi,
hivyo kuamua kuiuza kiholela ni jambo la kushangaza, ingawa pia si
dhambi kufanya hivyo kwa mtu yoyote kwa sababu ni biashara kama
zilivyokuwa biashara nyinginge," alisema.
Aidha
Kusaga aliwahakikishia Watanzania kuwa Clouds ni chombo huru
kisichofungamana na chama chochote cha siasa, huku akisema kwamba katika
Uchaguzi Mkuu mwaka huu haki itatolewa kwa vyama vyote na wanasiasa
wote.
“Huu
ni mwaka mgumu, hivyo naomba niseme ikitokea suala la kuhoji au kuunga
mkono siasa, basi haki itatolewa kwa wanasiasa wote, ukizingatia kwamba
chombo chetu hakika chama cha siasa inachokiunga mkono kwa sababu zozote
zile,” alisema Kusaga.
No comments:
Post a Comment