Breaking News:Mbunge wa Mbinga Mh.Kapteni John Komba afariki dunia ghafla - LEKULE

Breaking

28 Feb 2015

Breaking News:Mbunge wa Mbinga Mh.Kapteni John Komba afariki dunia ghafla


Mbunge wa Mbinga magharibi Mh.Kapteni John Komba amefarika ghafla leo katika hospital ya TMJ Mikocheni.

Kwa mujibu wa mtoto  wa marehemu Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kwamba sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach.

"Ni kweli mzee amefariki dakika hamsini zilizopita alikuwa nyumbani amekaa na mara ghafla sukari ikashuka na baadae kidogo alifariki,amesema Jerry Komba mtoto wa marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini alisema mbunge huyo alikimbizwa katika hospital ya TMJ ndipo umaiti ulipomkuta.Aidha bwana Gasper aliongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hospital ya lugalo jijini Dar es salaam na bado ratiba ya mazishi haijafahamika.

No comments: