Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika
vikali kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye
ni mume wa mwanamke aitwaye Sophia.
Mashuhuda waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya
tukio alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado
kumalizika.
Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.
“Alisema amelazimika kuondoka kwa Jose kwa sababu kitendo
alichokifanya kimemtia aibu kubwa. Kwamba haiwezekani yeye atulie
nyumbani Siku ya Wapendanao halafu mumewe akachepuke mitaani na mwanamke
mwingine,” kilisema chanzo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, Februari 14,
mwaka huu (Siku ya Wapendanao Duniani) kwenye Kitongoji cha Nyihongo
wilayani Kahama, Shinyanga wakati wadau mbalimbali walikuwa kila mtu na
wake.
Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.
“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba
inayojengwa. Yule mtu alishajua Jose anachepuka na yule mke wa jamaa,
akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia na kumnasa,” kilisema chanzo.
Chanzo kikaendelea kuweka wazi kuwa, baada ya Jose kunaswa
alitembezewa kichapo kizito na kupelekwa kwenye ofisi za serikali ya
mtaa ambapo Jose alipigwa faini ya shilingi laki tatu.
“Lakini
kilichotokea sasa ni kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose
naye kwa hasira aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kwao.
No comments:
Post a Comment