Shirika la haki za binadamu la
Amnesty International lenye makao yake makuu huko Washington Marekani,
limewataka wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa
kutotumua kura yao ya
turufu wakati maafa yanapotokea.Katika ripoti yake ya kila mwaka Amnesty International limesema kuwa mwaka wa 2014 ulikuwa ni mwaka ambao mamilioni ya watu walijikutaka kwenye matatizo makubwa zaidi lakini limesema kuwa hatua za kimataifa dhidi ya
hilo zilikuwa za kufedhehesha.
Shirika hilo limesema kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiweka maslahi ya nchi mbele kuliko maswala ya haki za binaadam.
Amnesty International imesema viongozi wa dunia walitakiwa kuchukua hatua mapema kushughulikia migogoro ambayo imewaacha Watu zaidi kulazimika kuishi chini ya udhibiti wa Makundi ya kigaidi kama vile Islamic State.
No comments:
Post a Comment