Wizara ya Ardhi yadaiwa kukiuka sheria za ardhi Tanzania - LEKULE

Breaking

16 Jan 2015

Wizara ya Ardhi yadaiwa kukiuka sheria za ardhi Tanzania


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya ya ardhi maliasili na mazingira Bw. James Lembeli.
Kamati ya Bunge ya ardhi maliasili na mazingira imeitaja wizara ya ardhi kuwa kinara wa urasimu na ukiukwaji wa taratibu na sheria za ardhi suala linalopelekea   kuchochea migogoro na ucheleweshwaji wa mikataba ya ardhi inayotekelezwa na mashirika na idara za serikali.
Kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya ya ardhi maliasili na mazingira Bw. James Lembeli mara baada kamati hiyo akitembelea eneo la uwekezaji wa shirika la nyumba NHC Mbezi luguluni jijini Dar es Salaam ambapo  ametaja mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kugawa ardhi mara mbili, kugawa maeneo ya wazi, hifadhi za mito, barabara, mabwawa pamoja na kukiuka sheria ya uendelezaji wa ardhi kwa kipindi cha miaka mitatu na kusababisha watu kuhodhi maeneo makubwa kwa muda mrefu bila ya kuyaendeleza kinyume cha sheria za nchi nchini Tanzania.
Naye  katibu mkuu wizara ya ardhi nyumba na makazi Bw. Alphayo Kidata amekiri mapungufu hayo na kueleza kuwa  yanachochewa na baadhi ya watendaji katika halasmashauri, manispaa na wizarani kushindwa kusimamia sheria na kanuni na kujikuta wakiiweka wizara katika wakati mgumu wa kutatua migogoro hiyo.

No comments: