Waziri:''Mashoga watibiwe ili waponywe India'' - LEKULE

Breaking

13 Jan 2015

Waziri:''Mashoga watibiwe ili waponywe India''



Pameibuka hasira kali miongoni mwa jamii ya Wagoa nchini India,wakati ambapo serikali ilipoamua kuweka bayana kuwa kutakuwa na vituo vya kuwaponya wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja.

Waziri wa michezo na mahusiano ya vijana Ramesh Tawadkar ameeleza kuwa tiba itatolewa kwa wanawake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja,wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsi amoja,wanaobadili jinsia zao,na wapenda jinsia zote mbili lengo ni kuwafanya warejee katika utu wao wa awali.

Baada ya tamko hilo jamii ya Goa ilihamishia mjadala katika mitandao ya kijamii huku walio wengi wakimpinga Tawadkar kwa matamshi yake ya kushtusha.

Mnamo mwaka 2013,mahakama kuu nchini India iliubadili uamuzi wa mahakama ya mwanzo kwa kuitupilia mbali sheria ya mkoloni kutoka Uingereza iliyodumu kwa takribani miaka 153,na kutoa tamko la kwamba nchini humo mapenzi ya jinsi moja ni kosa la jinai,na kuleta mjadala mkubwa ulimwenguni na huku wengine wakiuita uamuzi huo kuwa ni wa kufedhehesha.

Kwa muujibu wa kifungu cha 377 cha sheria za nchini India,mapenzi ya jinsi moja ni makosa makubwa kinyume na asili na ukikutwa na hatia hukumu yake ni miaka kumi jela.

Mwandishi wa BBC mjini Delhi anaeleza kuwa hata hivyo sheria hiyo haijaanza kufanya kazi kwa uzito unaostahili na badala yake polisi wamekuwa wakiitumia kuwanyanyasia wapenzi wa jinsi moja.

Nchini India wahafidhina wa kale ,ushiriki katika mapenzi ya jinsi moja ni mwiko na jamii ina mtazamo tofauti juu ya mahusiano hayo na huyachukulia kuwa ni haramu na tamko la waziri Tawadkar ni sawa na kuruhusu mahusiano hayo na kukinza fikra za wahafidhina.

Naye alisikika akisema tutawarejesha wapenzi wa jinis moja katika hali zao za awali.tutakuwa na kituo kwa ajili yao kama ambavyo wanaojaribu kujitoa katika ulevi wa kupindukia walivyo na kituo chao,tutawapatia mafunzo na kuwapa dawa pia,alisema waziri huyo mwenye dhamana,wakati akiwasilisha ripoti inayohusiana na vijana .

Makundi mengine ya vijana walengwa juu ya masuala ya vijana wahalifu,wanaotumia dawa za kulevya,waliotelekezwa na wahamiaji,vijana walioathiriwa na mazingira ripoti ihusianayo na vijana endapo itatoka itakuwa imeangazia changamoto zinazowakabili na namna ya kukabiliana nayo hasa suala la mapenzi ya jinsi moja.

Mtandao wa Twitter tangu mwanzoni mwa wiki hii umegubigwa na ujumbe mkali wenye kumkosoa waziri huyo kuhusiana na tamko lake.

No comments: