Watu 76 elfu wauawa nchini Syria 2014 - LEKULE

Breaking

2 Jan 2015

Watu 76 elfu wauawa nchini Syria 2014

Mwaka 2014 ulikuwa mwaka mbaya kuliko yote katika mgogoro wa Syria uliodumu kwa miaka minne, ambapo mwaka jana watu zaidi ya 76,000 waliuawa. Wanasema wanaharakati.

Shirika la Syrian Observatory la Haki za Binadamu lenye makao yake nchini Uingereza, limesema kati ya waliouawa 17,790 walikuwa raia wakiwemo watoto 3,501.

Wakati huo huo zaidi ya watu 15,000 walikufa katika mgogoro wa Iraq mwaka 2014, idadi ambayo inafanya mwaka 2014 kuwa mbaya kuliko yote katika mgogoro wa Iraq tangu mwaka 2007.


Mauaji mengi yametokana na kuongezeka kwa harakati za kundi la Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji katika nchi za Syria na Iraq.

Mashambulio ya anga yanayoongozwa na Marekani dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS), yanayopigana kati ya majeshi ya serikali na waasi nchini Syria, na ghasia za kidini nchini Iraq pia zimesababisha idadi kubwa ya vifo vya watu katika nchi mbili hizo.

Mashambulio ya anga yaliendelea Alhamisi, 17 yakilenga maeneo ya IS karibu na miji ya Raqqa, Kobane na Deir al-Zour nchini Syria na 12 karibu na miji ya Falluja, Mosul na Sinjar nchini Iraq.

Wakati huo huo Rais Bashar al-Assad wa Syria aliadhimisha sikukuu ya mwaka mpya kwa kutembelea vikosi vyake vya mstari wa mbele katika kitongoji cha Jobar mjini Damascus.

No comments: