Polisi nchini Pakistan wamekabiliana na waandamanaji, walioghadhabishwa na uamuzi wa jarida na Ufaransa la Charlie Hebdo wa kuchapisha vibonzo vya mtu wanayedai ni Mtume Mohammad.
Baada ya maombi ya ijumaa, maafisa wa ulinzi walitumia magari yenye majai kuwamwagia maji waandamanaji katika juhudi za kuwatwanya.
Walikuwa wamekusanyika nje ya ubalozi wa Ufaransa mjini Karachi.
Baadhi ya waandamanaji inaarifiwa walikuwa wamebeba bunduki. Watu watatu walijeruhiwa katika maandamano yenyewe.
Mwandishi wa BBC mjini Islamabad amesema idadi ya waandamanaji hao, kwa mujibu wa idadi ya wasisilamu nchini Pakistan, ilikuwa ndogo.
Maandamano kama hayo yameitishwa katika nchi zingine zilizo na idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu kama vile Uturuki, Ufilipino,Kuwait, Mauritania na Sudan.
No comments:
Post a Comment