Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa
kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya
zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika
kipindi cha miaka mitatu iliopita.
Kumbukumbu zilizopatikana na
gazeti la The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha
ongezeko la asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa kingono kwa kutumia
nguvu katika hospitali tangu mwaka 2011.Unyanyasaji huo unashirikisha visa 157 vya ubakaji.Takwimu za unyanyasaji huo katika hospitali zilitolewa na vituo 38 vya polisi kati ya vituo 45 nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment