Wachezaji kumi bora ulimwenguni wenye mapato ya juu - LEKULE

Breaking

20 Jan 2015

Wachezaji kumi bora ulimwenguni wenye mapato ya juu

Nambari moja

Rekodi yake haiwezi kushindaniwa. Mapigano 47, ameshinda mara 47. Floyd Mayweather Jr. ni nguli ulingoni, na shujaa wa biashara nje ya ulingo. Bingwa huyo wa ndondi za kitengo cha welterweight mwenye umri wa miaka 27 alipata dola milioni 105 mwaka jana, na kuwa mchezaji mwenye mapato ya juu zaidi ulimwenguni kwa mujibu wa jarida la Forbes.


Namba mbili
Ana kasi, anapendeza na ni tajiri

Cristiano Ronaldo ni mmoja wa wanakandanda wenye kipaji ulimwenguni na pia ni mmoja watu wanaopendeza. Hata akicheza mechi kwa dakika 90 katika mvua, CR7 atatoka uwanjani akiwa anapendeza. Haishangazi kuwa baadhi ya hereni zake inatoka kwa kampuni yake mwenyewe ya mitindo. Mapato yake ya mwaka ni dola milioni 80


Namba tatu

Mfalme James

Huku akipigiwa upatu tangu utotoni, Lebron James mwenye umri wa miaka 29 sasa tayari amejibadilisha na kuwa nguli wa mpira wa kikapu. Amepigiwa kura kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa katika ligi kuu ya Marekani - NBA mara nne mfululizo, na kando na kuwa balozi wa kimataifa wa mpira wa kikapu, mapato yake ya kila mwaak ni dola milioni 72.3.


Namba nne

Mchezaji wa nne ulimwenguni mwenye mapato ya juu, Lionel Messi, alianza kuwavutia watu akiwa na umri mdogo sana kuliko LeBron James. Akiwa chipukizi, Muargentina huyo alihamia katika klabu ya Uhispania ya Barcelona, ambako aliyanoa makali yake ya kandanda. Sasa ni nyota wa ulimwengu, akiwa na mapato ya dola milioni 64.7 kila mwaka kabla ya kukatwa kodi.


Namba tano

Sifa za nyota wa kuaminika

Taaluma yake katika NBA imekuwa ya kishujaa: Kobe Bryant amecheza wka miaka mingi katika ligi ya NBA, na amekuwa bingwa wa NBA mara tano. Mchezaji huyo wa klabu ya Lakers sasa ana umri wa miaka 36 na anasalia kuwa mmoja wa wachezaji nguli wa mpira wa kikapu. Juu ya hayo, bado anapata dola milioni 61.5 kila mwaka


Namba sita

Bilioneya wa golf

Tiger Woods anamzidi Kobe Bryant kwa miaka miwili, na kwa sasa hayuko katika kiwango kizuri zaidi cha taaluma yake lakini bado anatengeneza dola milioni 61.2 kila mwaka. Kiasi kikubwa hakitokei uwanjani bali matangazo ya kibiashara. Ndiye mchezaji wa kwanza katika historia kuwahi kupata dola bilioni moja, katika kipindi cha taaluma yake.


Namba saba

Fahari ya Uswisi

Wapinzani wake Novak Djokovic na Rafael Nadal huenda wamechukua udhibiti wa mchezo huo, lakini gwiji wa tennis Mswisi Roger Federer bado anafaidika katika ulimwengu wa tennis. Hata ingawa hajaongeza chochote karibuni kwa mataji yake 17 ya Grand Slam, orodha yake ya matangazo ya kibishara ndiyo sababu kubwa ambayo inampa kipato cha dola milioni 56.2 kila mwaka.


Namba nane

Faida kubwa ya mkono wake wa kushoto

Kando na mikutano ya karibuni ya waandishi wa habari baada ya mchezo, Phil Mickelson huenda ni mmoja wa wachezaji watulivu zaidi katika orodha ya kumi bora. Mwana golf huyo Mmarekani mwenye umri wa miaka 40 ameshinda zaidi ya mashindano 50 katika taaluma yake na amepata faida kubwa. Mapato yake ya kila mwaka ni dola milioni 53.2, na hiyo siyo mbaya sana.


Namba tisa

Bingwa asiyekata tamaa

Mkakamavu, mwepesi na mwenye mafanikio makubwa. Mbinu ya Rafael Nadal ya kucheza tennis haimpendezi mpinzani yoyote. Majeraha mara nyingi yamemweka mkekani nyota huyo wa tennis Mhispania, lakini anajikakamua vilivyo. Mafanikio yake hayatokei uwanjani tu. Mapato ya kila mwaka ya Mhispania huyo ni dola milioni 44.5


Namba kumi

Mashine ya kupeana pasi

Matt Ryan siyo mmoja wa wachezaji mashuhuri sana ulimwenguni. hata hivyo, mchezaji huyo wa soka ya Marekani anapata pesa nyingi kuwaliko Neymar, Lewis Hamilton na MS Dhoni. Mchezaji huyo wa klabu ya Atlanta anapata dola milioni 43.8 kila mwaka, hasa kutokana na mkataba aliosaini mwaka jana katika timu hiyo.







No comments: