Tanzania na mabadiliko ya tabia nchi - LEKULE

Breaking

22 Jan 2015

Tanzania na mabadiliko ya tabia nchi

Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa yakileta madhara duniani ,nchini Tanzanian mamlaka ya hali ya hewa imelazimika kutoa taarifa maalumu kwa umma kuhusiana na tahadhali ya mabadiliko ya hali hewa katika ukanda wa Pwani kutokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la Bahari ya hindi mashariki mwa kisiwa cha Madagascar hali inayoleta mawimbi makali.

Shughuli ya uvuvi katika bahari ya Hindi ni tegemeo kwa uchumi na huduma ya samaki,lakini kwa sasa mambo yamebadilika samaki wanapatikana kwa tabu kufuatia wavuvi kuogopa kuingia Baharini kuvua,huku hali ya usafiri kwa vyombo vya majini ndani ya Bahari hiyo vikikumbwa na hali mbaya kutokana na mawimbi makali.

Hali hiyo ya kuchafuka kwa bahari na hali ya hewa, pamoja na mawimbi makali bahari ya Hindi, ni kilio kikubwa kwa wavuvi wa mwambao huo wanaoendesha maisha yao kwa kutegemea uvuvi, kwani kwa sasa samaki hawapatikani tena kama hapo awali.
Hali ya mabadiliko ya tabia nchi, kwa mwaka huu wa 2015 limekuwa si jambo la kawaida, kwani kwa kawaida nchini Tanzaia majira kama haya ya mwezi wa kwanza mpaka wa pili katikati upepo hukata na kuwapa fursa wavuvi kutafuta riziki zao.

Kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa,imeathiri upatikanaji wa mazao ya samaki na sasa bidhaa ya samaki imepanda bei kutoka elfu kumi ama ishirini kwa ndoo ya lita kumi hapo awali sasa inauzwa kwa elfu sabini kwa dagaa mchele, na hivyo kumfanya mjasiriamali mwenye kipato cha chini kutomudu kununua bidhaa hiyo.

No comments: