Chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza ambacho kimekuwa kikipinga hatua
ya kubana matumizi kimeshinda katika uchaguzi uliofanyika nchini
humo,japo kuwa hakuna uhakika kama kina viti vya kutosha Bungeni kuweza
kuongoza serikali. Kiongozi wa chama cha Alexis Tsipras amewaambia
wafuasi wake kaytakia mji mkuu Anthens kuwa hatua ya kubana matumizi
iliyotangazwa na serikali inayoondoka imefikia mwisho na watafanya kazi
na wakopeshaji na kukubaliana namna ya kushughulikia madeni ya taifa.
Waziri mkuu anayeondoka madarakani Antonis Samaras amemtaka kiongozi wa
chama cha Syriza Alexis Tsipras kumpongeza. Samaras anadai kuwa sera
zake zilisaidia kufufua uchumi wa Ugiriki na kwamba walichukua hatua
kudumisha hali ya usalama wa raia. Amesema kuwa anakabidhi nchi ambayo
ni mwanachama wa umoja wa Ulaya na sarafu ya euro.
26 Jan 2015
New
Syriza yashinda uchaguzi,Ugiriki
About SOSTENES LEKULE JR
Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
KIMATAIFA
Tags
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment