Miongoni mwa story zilizochukua headline Jan 2 ni kuhusu kikundi cha vijana wa ‘Panya Road’ kuvamia maeneo mbalimbali, kupora vitu na kupiga watu.
Mwaka jana msanii wa filamu, Kajala Masanja alizindua filamu mpya ‘Mbwa Mwitu‘ iliyotengenzewa chini ya kampuni yake ya Kajala Entertainment, kulikuwa na baadhi ya washiriki ambao ni vijana waliokuwa wakijihusisha na matukio ya uhalifu.
Akizungumza na kipindi cha Take One ya Clouds TV, Kajala amesema; “Ilikuwa ni kazi ngumu sana kwani tuliwapa hela hata ya kutumia kidogo then tukawaomba hayo vijana walikiri kweli walikuwa katika hayo makundi maarufu kama Panya Road na Mbwa Mwitu basi tukawachukua tukaelekea nao location kutengeneza filamu yangu mpya ‘Mbwa Mwitu’ ambayo niliizindua mwaka jana Century Cinema, Mlimani City“, alisema Kajala.
Kwa upande wao washiriki ambao walikuwa wahalifu wamesimulia namna ambavyo walikuwa wakifanya matukio na baadaye wakaamua kuacha; “Katika maisha yetu ya uwizi tukaanza kufa mmoja mmoja yaani kadri ya mtu alipokuwa anazidi kufa mimi cheo kilikuwa kinazidi kupanda yaani akili inatanuka na matukio ya uhalifu ulikuwa unaongezeka, tushafanya matukio mengi tumeshatoka watoto wa watu sadaka wengi mpaka sasa hivi tumeshaepuka na ishu hizo tunamshukuru Mungu;’walisema vijana hao“-.
No comments:
Post a Comment