Mwenyekiti wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na kutisha yalitokea juzi saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga waliingia chumbani kwa marehemu na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.
Alisema baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawaka nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.
No comments:
Post a Comment