Saudi Arabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake.
Mwanablogu huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha mtandao wa 'Forum Liberal Saudi Network' ambao sasa umefungwa na serikali, alitarajiwa kuchapwa viboko 50 hadharani baada ya sala ya Ijumaa hii leo.
Mwezi Mei mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi 1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.
Bwana Badawi alipokea awamu ya kwanza ya viboko Ijumaa iliyopita huku kesi yake ikisababisha tuhuma kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali ya Saudia.
Hata hivyo serikali haikutoa tamko lolote kwa kukosolewa.
Kadhalika serikali hio ingali kutoa tamko kuhusu afya ya mwanablogu huyo na pia kuhusu kuahirishwa kwa adhabu yake.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International yamesema katika taarifa yao kwamba Badawi alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kugundua kwamba uchungu na majereha aliyoyapata kutoka kwa mijeledi ya kwanza bado hazijapona.
Daktari wake alishauri adhabu yake kuahirishwa hadi atakapopata nafuu
No comments:
Post a Comment