Msimamo wa Serikali: CUF inatafuta Umaarufu wa Kisiasa, Walikaidi Amri na ndo maana Wakapigwa - LEKULE

Breaking

29 Jan 2015

Msimamo wa Serikali: CUF inatafuta Umaarufu wa Kisiasa, Walikaidi Amri na ndo maana Wakapigwa



Akifafanua Bungeni kuhusu CUF kupigwa na Polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe amesema Chama cha CUF kilitimiza masharti yote lakini polisi ina haki ya kuzuia endapo itajiridhisha kuwa kuna uvunjifu wa amani.
Chikawe amesema CUF wakiongozwa na kiongozi wao walikaidi amri ya polisi, na ndiyo maana walipigwa.
Pia ameongeza kuwa CUF inatafuta umaarufu wa kisiasa na huruma ya wananchi.
"Jeshi la polisi halitamuogopa,kumhofia mtu,ninawaagiza polisi nchini kote kufanya kazi yao bila hofu wala kumuogopa mtu"- Chikawe

No comments: