Akaunti za ya Centcom ya Jeshi la Marekani za mitandao ya kijamii yaTwitter, facebook na Youtube imetekwa na kundi lilijitajwa kuwa na uhusiano na kikosi cha Ugaidi cha ISIS.
Kutekwa kwa akaunti hizo, mbali na kuliabisha Jeshi hilo lenye nguvu, uwezo katika nyanja mbali mbali na heshima duniani, pia kulipelekea akaunti hizo kufungwa kwa muda.
Watu walioteka mitandao hiyo waliacha ujumbe wenye vitisho kwa wanajeshi wa Marekani, huku pia wakiweka hadharani baadhi ya taarifa binafsi za baadhi ya Makamanda wa Jeshi hilo kama anuani wanakoishi na kadhalika.
Katika mtandao wa Youtube, wavamizi hao waliweza kuweka video yenye ujumbe wa vitisho na kejeli kwa Jeshi hilo.
Uvamizi wa akaunti hizo za Jeshi ulifanyika siku ambayo Rais Barack Obama wa Marekani alikuwa azungumzie unyeti wa suala za usalama wa technohama kwa nchi hiyo, huko akiainisha baadhi ya hatua ambazo nchi hiyo inategemea kuzichukuwa ili kushugulikia baadhi ya chanagamoto ambazo zimeshajitokeza.
No comments:
Post a Comment