Bossi wa Manchester City Manuel
Pellegrini amefungua milango ya kutaka kumsajili mshambuliaji Lionel
Messi toka Barcelona, ambapo wako tayari kuvunja benki kwa kutoa kitita
cha £480milioni.
Arsenal wako tayari kutoa £63milion kwa klabu
Borussia Dortmund ilikuweza kuwasajili nyota wawili wa timu hiyo kiungo
Ilkay Gundogan na beki Mats Hummels.Timu ya Palermo imekataa kukubali ofa ya kuumza mshambulaiji wake Paulo Dybala,kwa Manchester United mchezaji huyu anakadiriwa kuwa na thamani ya £30milioni.
Paris St-Germain, Porto na Juventus wanapigana vikumbo katika kutaka kumsajili kwa mkopo kinda Adnan Januzaj mwenye miaka 19 toka Manchester United.
Crystal Palace wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Bafetimbi Gomis, toka Swansea City kwa ada ya uhamisho ya £8milion.
Meneja wa West Brom Tony Pulis anataka kumsajili kiungo mkongwe wa Manchester United Darren Fletcher mwenye miaka 31, ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.
Swansea wanataka kutumia pesa walizopata kwa kuuza mshambuliaji Wilfried Bony kumsajili kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart ya Ujerumani
Manchester United wameanza mazungumzo na klabu ya PSG ili dau £30milion ili kumnasa la kumsajili mlinzi Marquinhos raia wa Brazil.
Kocha Jose Mourinho yuko tayari kuwatoa Andre Schurrle, na winga Mohamed Salah,il;I kupata pesa ya kumnunua beki Raphael Varane wa klabu ya Real Madrid.
Mshambauliaji wa Everton Kevin Mirallas amesema ataamua hatima mwishoni mwa msimu kama ataendelea kusalia Goodison Park au atahamia klabu nyingine.
No comments:
Post a Comment