Mhubiri mmoja nchini Iran amewaacha watu vinywa wazi kwa kuvalia vazi la rangi ya manjano.
Hoseyn Khademian alionekana kwenye televisheni akivalia shati la manjano , viatu na hata saa ya rangi hiohio. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr.
Wahubiri nchini Iran, kwa kawaida huvalia mavazi meupe na joho la rangi isiyong'aa sana huku viatu vyao vikiwa vyeusi au vya hudhurungi.
Lakini mavazi ya Khademian yalikejeliwa na kufanyiwa gumzo sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati baadhi ya watu kwenye Facebook walimzomea wakisema anajitakia tu sifa, wengine walimfananisha na ndizi lilioivaa kupitiliza. ''
Msomaji mwengine alisema, '' angependeza zaidi ikiwa angevalia kilemba cha waridi,basi angependeza sana''.
Wakati mwonekano wake umegonga vichwa vya habari nchini Iran, bwana Khademian anasema yeye haoni kwa nini watu wanamsema sana kwani sio mara yake ya kwanza kuvalia mavazi ya manjano.
Mara ya mwisho alionekana kwenye TV akiwa amevalia mavazi ya waridi, anahoji ''kwa nini watu hawakunisema sana wakati huo,''ikilinganishwa na sasa rangi ya mavazi yangi sio kitu kipya,'' alisema Bwana Khademian. Rangi ya manjano ni rangi ya kawaida kama rangi nyinginezo''.
No comments:
Post a Comment