Makasisi watatu wa kanisa la Baptist
nchini Guinea wamechapwa na kisha kutekwa nyara baada ya wenyeji
kuwashuku kuwa maafisa wanaohamasisha jamii dhidi ya ugonjwa hatari wa
Ebola.
Makasisi hao, walikuwa wametembelea kijiji cha Kabac eneo
la Forecariah wakilenga kufukiza dawa ya wadudu kwenye kuta za vyoo za
umma na katika sehemu za kuteka maji.Mwandishi wa BBC anasema kwamba wanakijiji hao punde tu walipowaona, waliwashuku kutaka kueneza ugonjwa wa Ebola katika eneo hilo.
Zaidi ya watu 8,600 wamefariki katika kanda ya Afrika Magharibi kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Mapema mwezi huu, wakazi katika eneo la Forecariah walishambulia na kuwaua polisi wawili walioshukiwa kuwa na njama ya kueneza Ebola katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment