Man United yatoka sare - LEKULE

Breaking

1 Jan 2015

Man United yatoka sare

Bingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Manchester United kwa mara nyingine wamezuiliwa na timu ya Stoke City katika mchuano uliokuwa wa kasi na kuchangamsha.

Man United ilipata sare ya 1-1 na hivyobasi kusalia katika nafasi ya 3 ikiwa na alama 37.

Stoke City ndio iliokuwa ya kwanza kufunga katika dakika ya 2 ya kipindi cha kwanza kabla ya mshambuliaji matata wa Manchester United Radamel Falcao kusawazisha baadaye.

Ijapokuwa timu zote zilionyesha mchezo mzuri Stoke City ilifanya mashambulizi mengi katika ngome ya Man United ikilinganishwa na mashetani hao wekundu.

Kunapo dakika za lala salama wachezaji wa Stoke City walilalama baada ya kudai kwamba refa aliwanyima mkwaju wa penalti baada ya beki Chris Smalling kuunawa mpira katika eneo la hatari.

No comments: