Akizungumzia kipaji chake cha uigizaji, Flora Mtegoa “Mama Kanumba” alisema hakufanya hivyo baada ya mwanaye kufariki, bali alikuwa akiigiza wakati alipokuwa kigori, hivyo ameamua kuendeleza kipaji chake.
“Nikiwa sekondari niliigiza, wakati huo mtoto wa kike kupelekwa shule mpaka vikao, zamani binti hakuruhusiwa kusoma, ilikuwa ngumu, kwa hiyo unacheza huku ukifikiria kwamba nyumbani wakijua nimeingia huku itakuwa tatizo, baadaye nikaacha,” alisema.
Alisema baada ya Kanumba kufariki, aliamua kuendeleza kipaji chake kwa kutumia rasilimali alizoachiwa na mtoto wake. Aliysema haya kwenye maojionao na Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment