Makataa ya FDLR kujisalimisha yakamilika - LEKULE

Breaking

2 Jan 2015

Makataa ya FDLR kujisalimisha yakamilika

Makataa yaliotolewa na mataifa ya maziwa makuu pamoja na jamii ya kimataifa kwa wapganaji wa Hutu nchini Rwanda FDLR kusalimisha silaha zao yanakamilika hii leo siku ya ijumaa.

Kufuatia kukamilika kwa ilani hiyo,oparesheni ya kijeshi itakayotekelezwa na jeshi la DRC na kusaidiwa na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa itaanzishwa ili kuwapokonya silaha kwa nguvu.

Kulingana na takwimu ni mmoja kati ya wapiganaji watano aliyesalimu kwa maafisa wa DRC,Kiwango ambacho kimedaiwa kuwa cha chini na mamlaka ya DRC,marekani pamoja na mataifa ya maziwa makuu.

No comments: