Mahakama kuu nchini India imeamrisha
kampuni kubwa za internet, Google, Yahoo na Microsoft kubana matangazo
ya biashara ya kuwapima wanawake wajawazito ili kubaini jinsia ya mtoto
kabla ya kuzaliwa.
Matangazo kama hayo, ni kinyume na sheria
nchini India kwa sababu kuna visa vingi vya wanawake kuavya mimba
wanapogundua wana mtoto mwenye jinsia wasioitaka.Hali hii imechochea tatizo la pengo katika jinsia moja kuwa ikilinganishwa na nyingine.
Mahakama ilikuwa inatoa uamuzi katika kesi iliyowasilishwa mbele yake kuhusu kuzagaa kwa matangazo ya biashara ya kubaini jinsia ya mtoto akiwa tumboni kwenye mitandao hio.
No comments:
Post a Comment