Mahakama nchini misri imebatilisha uamuzi wake kuhusiana na tuhuma za uproraji wa mali ya umma zilizokuwa zinamkabili aliyekuwa Rais wa wa nchi hio, Hosni Mubarak, na wanawe wawili.
Mahakama hio sasa inasema kesi hio itaanza kusikilizwa upya. Mahakama imemeelezea kuwa imegundua mikakati ya kisheria haikufuatwa.
Uamuzi huo una maana kwamba Mubarak ataondolewa katika hospitali ya kijeshi ambako anazuiliwa kwa mujibu wa wakili wake. Hio ndio kesi iliyoyokuwa imesalia mahakamani dhidi yake.
Mnamo mwezi Mei mwezi jana, Mubarak alikuwa emehukumiwa jela miaka mitatu kwa kupora mamilioni ya dola pesa ambazo zilinuiwa kuikarabati ikulu ya Rais.
Wanawe Mubarak, Gamal na Alaa,walifungwa jela miaka minne wakati hukumu ilipotolewa dhidi ya babao.
Tuhuma nyinginezo dhidi ya Mubarak ya kuamrisha mauaji ya waandamanaji mwaka 2011 wakati wa mapinduzi ya kiraia, zilitupiliwa mbali mwezi Novemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment