Kitendo cha kukamatwa,kupigwa kwa Mwenyekiti wa CUF, Prof.Ibrahim Lipumba kumesababisha sintofahamu leo kiasi cha bunge kuhairishwa hadi saa kumi jioni.
Akiwasilisha hoja hiyo Mh.James Mbatia alimwomba spika wa bunge kuruhusu bunge lijadili sababu za kupigwa kwa Prof.Lipumba, hasa akitaka kujua kufuatilia kauli ya jeshi la polisi kuwa walitekeleza amri ya ngazi za juu serikalini hivyo ijulikane kauli hiyo ilitolewa na nani huko ngazi za juu.
Kimbembe kilianza pale ambapo spika wa bunge alipokataa kujadiliwa leo na kusema kuwa anaiagiza serikali kuleta ripoti hiyo kesho na jambo hili kujadiliwa kesho sio leo,ndipo wabunge wa upinzani waligoma wakitaka ijadili leo na sio kesho hapo ikatokea sintofahamu na kelele kila mmoja akisema lake na ndipo spika alipoamua kuhairisha bunge hadi leo jion saa kumi.
No comments:
Post a Comment