Hofu ya Ebola kuwa sugu kutibu - LEKULE

Breaking

29 Jan 2015

Hofu ya Ebola kuwa sugu kutibu



Wanasayansi wanaokabiliana na janga la Ebola nchini Guinea wanasema kwamba virusi vinavyosababisha ugonjwa huo vimeanza kujibadilisha umbo na kuwa sugu hali inayoifanya vigumu kutibu ugonjwa wa Ebola.

Jambo hili linashuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu tangu ugonjwa huo kugunduliwa mwezi Machi mwaka jana.

Watafiti katika taasisi ya Pasteur mjini Paris Ufaransa, wamekuwa wakichunguza mamia za sampuli za damu kujaribu kubuni mbinu za kupambana na virusi hivyo.

Kwa sasa wanajaribu kubaini ikiwa kujibaidili kwa umbo virusi hivyo, kutasababisha maambukizi zaidi na ikiwa wanaweza kufanya lolote kuhusu ambavyo ugonwja huo unapimwa mwilini na pia ambavyo madawa yanatumika mwilini kupambana na ugonjwa huo.

Pia wanataka kuchunguza na kufanyia utafiiti chanjo dhidi ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola umewaua watu ziadi ya elfu nane huko magharibi mwa Afrika, wengi kutoka Guinea , Sierra Leone na Liberia

No comments: