Hina ( Heena ) ni aina ya urembo ambao umekuwa ukitumiwa na watu wengi hapa nchini Tanzania hususani katika maeneo ya pwani.
Kwa mujibu wa wataalamu wa Hina wanasema kuwa zipo aina mbalimbali za michoro ya hina kila moja ikiwa na muonekano tofauti na nyingine.
Hata hivyo mara nyingi aina hizi hutofautiana kulingana na mteja, mfano hina ya mtu anayetaka kufanya harusi ni tofauti kabisa wasichana au akinamama wa nyumbani.
Nianzie kuzungumzia aina ya Hina ya harusini,Hina hii huwa na maua makubwa na yaliyojaa tofauti na mingine. Si hivyo tu michoro hiyo huchukua sehemu kubwa ya maungo. Kwa mfano ikiwa ni mikononi, basi hupakwa hadi kwenye viwiko au kuanzia chini hadi juu kabisa
Katika hatua nyingine Hina kwa Wanaume hujulikana kama tattoo.Wanaume hupenda kuchora juu kabisa ya mkono.
Hata hivyo kwa upande wa watoto, hina hutumiwa na watoto hususan wa kike katika sikukuu hasa za Kiislamu kama vile Eid na Maulid
No comments:
Post a Comment