Siku ya jana January 12 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha alikuwa katika mahojiano katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV hapa kuna kile alichokizungumza kuhusu ishu ya kukwepa Kodi na Rushwa, msimamo wake kugombea Urais 2015 na ishu ya wahusika waliochukua Fedha za Escrow.
“Kwa nchi yetu, upande mmoja wa hili la kukwepa kodi na upande wa rushwa ukitaka kukomesha na lenyewe linasubiria Katiba Mpya tutakapokwenda kwenye Sheria hili tutasimamia mpaka koo litakauka… Yaani mtu kupokea rushwa anatakiwa anatakiwa akikadiria hivi siku nikipokea rushwa nikikamatwa madhara yake ni nini…“– Mwigulu Nchemba.
Anatakiwa ajue siku ileile kwamba hakuna dhamana, taratibu za kimahakama zitaendelea akiwa ndani nakutoka hapo adhabu yake inatakiwa imtishe… Kama mtu amesababisha hasara ya bilioni thelathini, kama adhabu nii kumuondoa tu kwenye nafasi aliyokuwa nayo umempa likizo akatumie fedha… Umempa send-off akasherekee fedha ya umma…”– Mwigulu Nchemba.
Taarifa nilizonazo tayari Mamlaka ya Mapato imeshafanya hesabu… Kuhusu haya mambo ya Kodi kweli tumedhamiria, kwamba lazima kodi ilipwe na hili si jambo la mjadala… Hatuwezi tukasamehe kodi kubwa vile halafu tukakimbizana na mama anayeuza mchicha…”– Mwigulu Nchemba.
Msimamo wangu kwenye masuala ya msingi yanayohusu taifa letu huwa hauyumbi wanaonifahamu wanajua…”
No comments:
Post a Comment