Ethiopia :Viongozi Afrika wakutana leo - LEKULE

Breaking

30 Jan 2015

Ethiopia :Viongozi Afrika wakutana leo

Viongozi barani Afrika wanafanya mazungumzo kuhusu hali ya Bara la Afrika

Mkutano wa wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika unaanza leo nchini Ethiopia ambapo viongozi wa Afrika wanatarajiwa kujadili masuala muhimu yanayolikumba bara la Afrika kwa sasa.

Wakati huo huo Kenya inatarajia kutuma ujumbe mzito kwenye mkutano huo kama mwanzo wa hatua yake ya kukata uhusiano na Mahakama ya jinai ICC.

Katika kikao cha Umoja wa Afrika kilichokaa mjini Malabo Equatorial Guinea wajumbe walisaini mkataba wa uundwaji wa mahakama ya Afrika itakayoshughulikia kesi za Afrika badala ya kuzipeleka kwenye mahakama ya ICC, baadhi yao wakidai kuwa kesi za mahakama hiyo zinawalenga waafrika pekee.

No comments: