Msanii anayetesa katika mziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa jumamosi iliyopita alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kuzomewa, Diamond pia alirushiwa chupa za maji ambazo zilileta kadhia, lakini Diamond alionekana akiwahimiza madancer wake wafanye kazi iliyowapeleka pale licha ya zomeazomea kuzidi uwanjani.....
Msanii huyo alipoona vitendo vya kutaka kumkwamisha asiimbe vikiendelea, aliamua kuwamwagia fedha mashabiki hao, ndipo wakaacha kuzomea na kuanza kugombea fedha hizo kisha kuanza kumshangilia....
Baadhi ya wadau walisikika wakidai, kundi hilo lililokuwa likimzomea liko upande wa mmoja wa wasanii mahiri hapa nchini.Wasanii wengine walioonja joto ya jiwe ni pamoja na Khamis Mwinjuma 'Mwana FA' na Ambwene Yesaya 'AY'.
Aidha, baadhi ya mashabiki walilaani vikali tukio hilo la kumzomea Diamond na kumrushia chupa za maji ambazo inadaiwa zilikuwa na haja ndogo ndani yake.
Mashabiki hao walisema tukio hilo halipendezi na linapaswa kukemewa na kuwataka waratibu pamoja na jeshi la polisi kuzidisha ulinzi katika matamasha makubwa kama hayo.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuzomewa,tukio la kwanza likiwa kilele cha tamasha la Fiesta mwaka jana kwenye viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment