Ban Ki Moon akemea machafuko, Nigeria - LEKULE

Breaking

13 Jan 2015

Ban Ki Moon akemea machafuko, Nigeria



Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amekemea machafuko yanayoendelea nchini Nigeria.Kauli ya Ban Ki Moon imekuja baada ya Ripoti kuwa mamia ya watu waliuawa mjini Baga katika jimbo la Borno. Pia ripoti kuhusu wanawake waliojitoa muhanga.

Ban Ki Moon amesema amesikitishwa na Ripoti zinazosema kuwa mamia ya Watu wameuawa mjini Baga.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekemea vitendo vya mashambulizi vinavyotekelezwa na Boko Haram.

Mji wa Baga ulishambuliwa na Wanamgambo siku tisa zilizopita.

Tangu kukimbia kwa wakazi, wakazi waneripotikuwa mamia ya watu waliuawa na sehemu kubwa ya mji huo ilichomwa moto.

Kulikua na mashambulizi kadhaa ya kujitoa muhanga kaskazini mwa Nigeria.

Maafisa wamesema aliyejitoa muhanga na kusababisha Watu 19 kupoteza maisha mjini Maiduguri alikuwa mtoto mdogo wa miaka kumi.

Wanawake wawili wanaokisiwa kuwa na miaka ya ishirini walijilipua bomu kwenye soko mjini Potiskum katika jimbo la Yobe.

Mwishoni mwa juma lililopita Jeshi la Nigeria lilipigana na Boko haram ambao walikuwa wakijaribu kuuteka mji wa Damaturu.

No comments: