Nahodha wa timu Ghana Asamoah Gyan anaugua maradhi yanayosemekana kuwa ni malaria na huenda asikipige na Senegal leo.
Shirikisho la soka la Ghana limetoa maelezo kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amepumzishwa hospitali katika mji wa Mongomo tangu Jumamosi jioni na kuruhusiwa Jumapili asubuhi ,na inaelezwa kuwa maradhi hayo yametibiwa katika hatua za awali na mchezaji huyo anaendelea vyema.
Na upande wa Senegal,Alain Giresse anapaswa kufanya maamuzi juu ya afya ya Sadio Mane, ambaye alikuwa nje ya dimba kutokana na kigimbi chake kuumia.Sadio ni mchezaji wa timu ya Southampton na alijumuishwa katika kikosi cha Senegal pamoja na kwamba timu yake iligoma kwa maelezo kwamba hatakuwa sawa kiafya.
Lakini Giresse ameendelea kushikilia msimamo wake kwa kusema kama hataweza kucheza katika mechi za awali,itakuwa maraya ya pili kama si ya tatu tutaangalia maendeleo ya hali yake.
Jina moja kubwa linalokosekana katika kikosi cha Senegal,ni mchezaji wa timu ya West Ham mshambuliaji Diafra Sakho,ambaye alikuwa na maumivu ya mgongo na hakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Senegal.Hata hivyo mchezaji mwenziwe wa timu ya Upton Park Cheikhou Kouyate yeye ataungana na kikosi hicho.
Kwa upande wake Sadio yeye,anaeleza kuwa alikuwa na ndoto ya kuichezea timu yake ya taifa katika kombe hilo la mataifa ya Afrika na kipaumbele ni timu ya Taifa na West Ham baadaye.kwa heshima alonayo kwa klabu yake,wanaheshimu uamuzi wake endapo kama asingekuwa na maumivu hayo, ni fursa pekee ambayo mtu yeyote asingependa kuikosa.
Kukosekana kwa Gyan katika kikosi cha taifa lake, yaeza kuwa mtihani kwa kocha wake mpya mGhana Avram Grant aliyewahi kuwa boss wa Chelsea lengo lake ni kuona Black Stars hawafungiki katika michuano hiyo dhidi ya Senegal.
Lakini walau analo chaguo, anaweza kumwita mchezaji wa timu ya Marseille ,mchezaji wa mbele Andre Ayew na pia mchezaji wa timua ya Everton Christian Atsu ama hata Mubarak Wakaso wa timu ya Celtic.
No comments:
Post a Comment