Arsene Wenger:''Vibali vya kazi vifutwe'' - LEKULE

Breaking

23 Jan 2015

Arsene Wenger:''Vibali vya kazi vifutwe''

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye umoja wa ulaya zifutwe.
Wenger anaejaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambae anahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake.
Bosi huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezajitoka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya wenye pasipoti katika michezo ya ligi ya England msimu ujao.
Akasema "Kusema ukweli inapaswa funguliwa kabisa, na kila mtu anaweza kungia"
Kwasasa kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo umoja wa Ulaya kunahitajika kuwa katika nafasi 70 za juu katika ubora wa viwango vya Fifa na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili.
"Ili kumsajili Paulista tungeweza kuwashawishi maofisa wa kwao kuwa ni beki wa kipekee mwenye kipaji."
Chama cha Soka cha Englan kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa jumuiya ya ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi.
Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora kwa ajili vijana wachezaji Kiingereza.
"kufunga mipaka ya nchi na kuruhusu kucheza wachezaji wa Kiingereza tu Nini kitatokea? Ni kuua mvuto wa ligi dunia kote.
Wenger alisema Arsenal walitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Ajentina Angel Di Maria lakini kibali cha kazi kikaleta shida.
Wenger aliongeza "Tulimtambua Di Maria alipokuwa 17.Tulimuona akiwa katika mashindano ya kimataifa na tulitaka aje hapa.
"Lakini alikwenda Ureno, na kutoka Ureno alikwenda Hispania. Kwa nini? Kwa sababu hakuweza kupata kibali cha kufanya kazi England.

No comments: