AFCON: Congo& Burkina Faso wasaka malazi - LEKULE

Breaking

15 Jan 2015

AFCON: Congo& Burkina Faso wasaka malazi

Kocha wa Congo Claude le Roy




Mambo yameanza kuiva na joto kupanda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa maarufu kama AFCON na kikubwa zaidi hivi sasa timu zote zinazo tia maguu Equatorial Guinea zinapaswa kutafuta mahala pa kuweka ubavu kwani kwa sasa pa kulala ni shiida .

Kocha wa timu kutoka Congo Claude Le Roy ,anathibitisha kuwa kwa upande wake washiriki kutoka nchini mwake wapatao 35 hawana vyumba vya kulala.

Kubwa zaidi Claude anasema hoteli waliyofikia haina hadhi na viwango vya msafara wake, na mbaya zaidi hoteli waliyofikia ina uhaba wa maji na nyaya za umeme ziko wazi zenye kutishia usalama wa watu wake waliofurika kwenye hotel hiyo na watano kati yao hawajui watalala wapi.

Sintofahamu hii haiko kwa timu ya Congo tu bali hata kwa timu kutoka Burkina Faso ,kwani kocha wao Paul Put, jicho lake limefanikiwa kuona vifaa duni vilivyoandaliwa kwa michuano hiyo, na kupendekeza kwamba ikiwa hali ni hiyo kuna sababu gani kuharakisha michuano hiyo na badala yake waahirishe mpaka mwezi June mwaka huu.

Equatorial Guinea yenyewe inakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Africa kwa taarifa ya papo hapo baada ya Morocco kuvuliwa haki ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwezi November.

Morocco ilisita kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa muda wa wiki tatu kwa hofu ya masuala ya kiafya kufuatia mripuko wa gonjwa la kutisha lililokuwa likiitatiza dunia Ebola .

Mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo itakuwa kati ya Congo na Equatorial Guinea siku ya Jumamosi na mchezo huo utapigwa katika mji wa Bata.

Akizungumza na BBC kocha Le Roy amethibitisha kuwa hali imeanza kutishia Amani kwani hakuna pa kulala na kuna ugumu wa kupata mahali pa malazi kwa maofisa wake na hata wachezaji wanaotakiwa wapumzike zaidi pia hawana pa kulala.

Umeme nao ni majanga,kila kitu kiko nje nyaya hazijavaa nguo zake,nikataka kuosha mikono yangu,hakuna maji.baadhi ya maafisa wangu nao walianza kuuzunguka mji wa Bata kuangalia kama watabahatisha pa kulala popote pale lakini imekuwa ngumu mno .

Uwanja wa Estadio de Bata utakuwa mwenyeji wa nusu fainali za michuano ya mwaka 2012.

Le Roy akazidi kusema kuwa pamoja na wakati mgumu unaowakabili wa kusaka malazi mpaka sasa hawajasaidiwa chochote na shirikisho la soka barani Afrika- CAF ,nay eye pamoja na maofisa wake walifika mjini humo siku moja kabla wakijihami wasije kumbwa na matatizo lakini hali imekuwa mbaya zaidi.

Haya niyaonayo niliyategemea,na sihitaji hoteli ya hadhi ya nyota tano,nnachotaka ni mahala safi pa kulala basi

Pamoja na hayo yote Le Roy amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanashinda katika kundi lao na hivyo watapata hotel nzuri ya kulala wakati walioshindwa watakapokuwa wakirejea makwao .

Lakini wachezaji wake tayari wameanza kukata tamaa na hasira juu kutokana na maandalizi duni waliyokutana nayo.

Michuano hii itaanza kupigwa rasmi Jumamosi na kufikia tamati tarehe 8 mwezi February.

No comments: