Wiki chache baada ya kujifungua mtoto wa kiume, msanii huyu kapatwa msiba wa mama yake mzazi… - LEKULE

Breaking

4 Dec 2014

Wiki chache baada ya kujifungua mtoto wa kiume, msanii huyu kapatwa msiba wa mama yake mzazi…


Ilikuwa furaha kubwa kwa ndugu, jamaa na marafiki wake wa karibu pale alipojifungua mtoto wa kiume wiki chache zilizopita.
Furaha yake haikuwa hapo tu, ila iliongezwa na tukio la ndoa ya binamu yake, lakini taarifa iliyoripotiwa jana kwamba mama yake mzazi ambaye jina lake ni Doris Rowland ni taarifa ya majonzi kwa wale wote walio karibu na familia hiyo.
Huyo ni mama mzazi wa msanii Kelly Rowland, na taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia imesema Doris amefariki Atlanta, Marekani akiwa na umri wa miaka 66.
Katika maelezo aliyoyatoa Kelly Rowland amesema mama yake alikuwa mtu aliyekuwa na moyo wa kujitoa zaidi kwenye maisha yake mpaka kwenye hatua aliyoifikia sasa.
It is with deep sadness that I announce the passing of my mother, Doris Rowland Garrison. She was an incredible soul who made countless sacrifices so that I could become the woman—and now mother—I am today,”
“We humbly appreciate all the love and support and only ask for privacy during this difficult time.“– Kelly.

No comments: