Watu kadha wauwawa karibu na Beni DRC - LEKULE

Breaking

8 Dec 2014

Watu kadha wauwawa karibu na Beni DRC


 Inaarifiwa kuwa watu kama 30 waliuwawa katika mashambulio kwenye vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Inaarifiwa kuwa mashambulio hayo yalifanywa Jumamosi usiku kwenye vijiji karibu na mji wa Beni ambako watu zaidi ya 250 wameuwawa tangu mwezi Oktoba.

Wakuu na mashirika ya raia yanawalaumu wapiganaji kutoka Uganda wa kundi la ADF, lakini baadhi ya wadadisi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha kundi hilo.

No comments: