Wahamiaji 70 wafa maji Yemen - LEKULE

Breaking

8 Dec 2014

Wahamiaji 70 wafa maji Yemen

Watu 70 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imejaza wahamiaji haramu kupinduka baharini, magharibi mwa Yemen.

Maafisa nchini Yemen wamesema wengi ya watu waliokuwa katika boti hiyo ni raia wa Ethiopia.

Hali mbaya ya hewa inaelezwa kwamba ndio chanzo cha kuzama kwa boti hiyo.

Mamia kwa maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa safari zisizo na usalama katika nchi zilizo katika pembe ya Afrika na Yemen kila mwaka.

Umoja wa Mataifa unamini kwamba kiasi cha watu watu mia mbili wamezama maji katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita.

No comments: