Mwigizaji azabwa kofi kwa kuvalia nguo fupi - LEKULE

Breaking

1 Dec 2014

Mwigizaji azabwa kofi kwa kuvalia nguo fupi


Mwigizaji maarufu wa Bollywood ambaye pia ni mwanamitindo, Gauhar Khan, alizabwa kofi wakati wa shughuli ya kurekodi makala ya kipindi kuhusu maisha yake.

Mwigizaji huyo alizabwa kofi na mmoja wa waliokuwa wanatazama kipindi hicho eti kwa kuwa alikuwa amevalia nguo fupi sana.

Polisi walimkamata mwanamume mwenye umri a miaka 24 kwa kumshambulia mwigizaji huyo wakati wa kurekodi kipindi kijulikanacho kama , ''India's Raw Star'' mjini Mumbai.

Mwanamume aliyemshambua muigizaji huyo alinukuliwa akimkaripia na kumwambia, kwamba kwa kuwa yeye ni mwanamke wa kiisilamu hapaswi kuvalia nguo fupi kama ile.

Mwanamume huyo alitarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Tukio hilo lilitokea Jumapili, wakati wa kurekodiwa kwa makala ya mwisho ya kipindi hicho.

Uchunguzi umeonyesha kuwa mtu mmoja kutoka kwa mashabiki, alianza kumkejeli Khan ambaye naye hakumsaza kwani alianza kujibizana naye. Katika majibizano yao, mwanamume huyo alimzaba kofi Khan.

Duru zinasema kuwa walinzi waliokuwa katika eneo hiloi walimshinda nguvu mwanamume huyo ambayo walimkabidhi kwa polisi.

Polisi walimshitaki mwanamume huyo kwa kitendo cha kumzaba kofi Khan ambaye ameigiza katika filamu nyingi tu ikiwemo, 'Rocket Singh: Salesman of the Year.'

No comments: