Mwanamume ajibandika urembo kufanana na Kim - LEKULE

Breaking

20 Dec 2014

Mwanamume ajibandika urembo kufanana na Kim



Sura huonekana katika baadhi ya majarida maarufu duniani, ana kipindi chake maalum kuhusu maisha yake na familia yake, ana kampuni ya vipodozi na pia ana mamilioni ya dola kwenye akauti zake za benki.
Si mwingine bali ni mwanadada Kim Kardashian ambaye yumo vinywani mwa watu wengi duniani.
Sio ajabu kama kuna mtu angetaka kufanana na yeye. Kutana na kijana Jordan James kutoka Uingereza mwenye umri wa miaka 23 ambaye ari yake maishani ni kufanana tu kama Kim Kardashian.
Mvulana huyu amefanya mambo ya ajabu akijitahidi kufanana na Kim kwa kujiongeza urembo bandia, hasa kufanya midomo yake kuwa mikubwa akitaka ifanane na ya Kim.
Je unajua ametumia kiwango gani cha pesa katika harakati zake za kutaka kufanana kama Kim? Pauni 150,000 au dola laki mbili na arobaini.
Pesa hizo zote amezitumia kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezwa urembo bandia.
Cha kushangaza ni kwamba huyu ni mwanamume anayetaka kufanana kama mwanamke
Amekua akitazama mamia ya picha za Kim akipiga pozi kumuiga

Aliambia jarida la The Sun kwamba alianza kumuenzi Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 33 baada ya kutazama makala ya kipindi kijulikanacho kama ''Keeping Up With The Kardashians.'' Kipindi kinachohusu Kim na Familia yake.

'ninapenda kila kitu kumhusu Kim,' aliambia The Sun. 'yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi duniani. Ngozi yake ni nyororo, nywele zake zinapendeza yaani kila kitu kumhusu kinanipendeza. ''

Jordan amefanyiwa upasuaji kuongeza urembo bandia zaidi ya mara 50 katika juhudi zake za kutaka kufanana kama Kim, amerembeshwa midomo, ametolewa nywele kwa kutumia miale ya Laser , amewekwa Tatoo na hata kubadilisha kope zake na mengine mengi.

Lakini mabadiliko haya yote yamemgeuza sura sana Jordan na kumanya kuwa kichekesho kwa watu wengi.

''Mimi mwenyewe hucheka watu wanapojaribu kunitusi au kunikejeli, na kuniambia kwamba mimi ni kama tu plastiki, yaani kila kitu mwilini mwangu ni baandia. Lakini hio hainijalishi.''

No comments: