Mtandao wa Korea kazkazini ulizimika kwa masaa kadhaa na kuzua uvumi kwamba huenda Marekani imeanza kulipiza kisasi kufuatia madai ya uhalifu wa mtandaoni uliofanyiwa kampuni moja ya filamu nchini Marekani.
Kulingana na kituo cha habari cha AFP haijulikani ni nani ama nini kilichozima mtandao wa Pyongyang ,lakini wataalam wa mitandao wamesema kuwa mtandao wa taifa hilo ulizima usiku kucha kutoka siku ya jumatatu hadi jumanne.
Wachanganuzi wa mtandao nchini Marekani Dyn Research wanasema kuwa kampuni nne za mtandao za Pyongayang zinazopata mtandao wake kutoka kwa kampuni ya mawasiliano ya Uchina, China Unicom zilikuwa zimezimwa kwa masaa tisa na dakika 31 kabla ya huduma kurejea siku ya jumanne.
Kampuni ya Dyn Research imesema kuwa mitandao michache iliopo Pyongyang huenda ikaathiriwa na kukatika kwa umeme lakini vile ilivyozimika kunazua mjadala kwamba huenda mitandao hiyo ilizimwa kutoka nje
Rais wa Marekani Barrack Obama na shirika la ujasusi la FBI limeishtumu Korea Kazkazini kwa kushambulia mitandao ya kampuni ya filamu ya Sony Pictures ambayo ilitishiwa na kuilazimu kuahirisha maonyesho ya filamu inayomkejeli rais wa taifa hilo Kim Jong-un.
Maafisa wa Washington wamekataa kutoa tamko kuhusu madai kwamba kuzimwa kwa mtandao wa Korea Kazkazini ni hatua ya kwanza ya rais Obama aliyeonya kwamba atalipiza kisasi shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment