Kenyatta:Kenya haitatikiswa na magaidi - LEKULE

Breaking

2 Dec 2014

Kenyatta:Kenya haitatikiswa na magaidi


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa Kenya haitachoka katika vita vyake dhidi ya ugaidi kufuatia shambulizi lililofanywa dhidi ya wachimba migodi mjini Mandera Kaskazini ya Kenya.

Ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa taifa baada ya shambulizi lengine lililofanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab dhidi ya wakenya wasiokuwa na hatia.

Kundi hilo liliwavamia wachimba migodi 36 waliokuwa katika machimbo ya kokoto mjini Mandera.

Kundi hilo liliwaua wakenya wengine 28 waliokuwa wanasafiri kutoka mjini Mandera siku kumi zilizopita.

Kenyatta amelaani wanamgambo hao wa Al Shabaab kwa kutaka kuigawanya Kenya katika msingi ya kidini na kuwataka wakenya kuungana dhidi ya kile alichokitaja vita dhidi ya ugaidi.

Kenyatta aliwataka magaidi wa Al Shabaab kama wanyama walio na kichaa.

Aliwasihi wakenya kuungana katika vita dhidi ya magaidi.

Siku kumi zilizopita, Al Shabaab waliuwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri kwa basi kutoka mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia kuelekea likizoni makwao. Wengi wa waliouawa walikuwa walimu wa shukle za umma. 

No comments: