Utafiti kuhusu uchaguzi ujao ni halisi? - LEKULE

Breaking

14 Nov 2014

Utafiti kuhusu uchaguzi ujao ni halisi?


Matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi huru isiyo ya kiserikali, nchini Tanzania TWAWEZA, kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa yaliyotangazwa wiki hii, yamepokelewa kwa maoni tofauti, hususan katika kipengele cha mgombea wa nafasi ya urais ambaye angechaguliwa iwapo uchaguzi ungefanyika katika siku ya utafiti huo.

Katika kipengele hicho Edward Lowassa waziri mkuu wa zamani wa Tanzania na waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda wote wawili kutoka chama tawala cha CCM ndio walioongoza katika utafiti huo kama wanavyofuatana, huku katibu mkuu wa chama cha Chadema, Dk. Wilbrod Slaa akishika nafasi ya tatu.

Mara baada ya kutolewa matokeo ya utafiti huu, watu mbalimbali wametoa maoni yao kuhusu usahihi na uhalali wa utafiti huo. Baadhi ya waliotoa maoni yao wameunga mkono utafiti wa Twaweza kuwa umetoa dira kwa wananchi na wanasiasa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka kesho endapo watataka kuchaguliwa au kupoteza nafasi walizonazo sasa.

Mwananchi mmoja kati ya watatu ambayo ni sawa na asilimia 33 kwa upande wa Tanzania Bara hajui ni nani atayekuwa chaguo lake la Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hakuna mgombea hata mmoja anayependwa na wapiga kura kwa zaidi ya asilimia 15%. Kwa maana hiyo nafasi hiyo iko wazi kwa kila mgombea. Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Twaweza mwezi Septemba 2014, anayeongoza ni Edward Lowassa akiwa na silimia 13% akifuatiwa na Mizengo Pinda asilimia 12 wote wa CCM, na watatu ni Dkt. Wilbrod Slaa wa Chadema asilimia 11.

Dk.Wilbrod Slaa ni mmoja wa waliotajwa katika utafiti huo ameongea na BBC akimesema umekosa mbinu za kisayansi katika kutoa matokeo sahihi.

Utafiti huo unasema Wafuasi wa CCM walipohojiwa, robo yao (24%) walisema watampigia kura yeyote atakayeteuliwa na chama.

Ukilinganisha kukubalika kwa vyama, nusu ya Watanzania (54%) wamesema wataipigia kura CCM kwenye uchaguzi wa Rais, na robo moja ya Watanzania (23%) wataipigia kura CHADEMA. Walipoulizwa watafanya nini kama vyama vya upinzani vitaungana na kusimika mgombea mmoja tu, kama UKAWA ilivyoahidi kufanya, CCM bado inaongoza lakini idadi ya watakaoichagua CCM inapungua hadi chini ya nusu (47%) ya wananchi wote. Wakati huohuo, karibu wananchi watatu kati ya kumi (28%) wamesema wangempigia kura mgombea wa upinzani. Idadi kubwa ya wananchi, mmoja kati ya watano (19%) amesema hatapigia kura chama bali mgombea. Ikitokea kundi hili likaamua kumpigia kura mgombea wa upinzani, ushindani utakuwa mkali mwaka 2015.

No comments: