Unamfahamu Doreen Kabuche?
Huyu ndiye mwanafunzi aliyekuwa
mwanafunzi bora wa kike kwa mwaka 2011 alipomaliza kidato cha sita Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa Dar es Salaam, lakini mwaka 2014
ameendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri katika masomo ambapo amekuwa
mwanafunzi bora kwa mara nyingine kwa kufaulu kwa GPA ya 4.8 kwenye
shahada ya Takwimu Bima.
Alichokiandika Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa siku ya leo ni hiki; “..Tulimwita
na nikamzawadia laptop ya 1,500,000. Mwaka huu amekuwa best student
UDSM kwa kupata GPA ya 4.8 kwenye Shahada adimu ya Takwimu Bima. Nataka
tumsomeshe Masters ili kupata wataalam watakaoangalia mifuko yetu ya
Pension, Tuache kulalamikia utendaji mbovu wakati hatusomeshi wataalam…“
No comments:
Post a Comment