Kwenye historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kuna historia nyingine inaandikwa ambapo Mbunge mwingine amefunga Ndoa leo.
Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………”
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”
Yes.. Ni kweli.. Mbunge huyo amefunga ndoa leo Kigoma, ujumbe alioandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka akiwa na Wabunge Deo Filikunjombe, Mwami na David Silinde.
No comments:
Post a Comment